Jumapili, 5 Aprili 2020

ATHARI ZA UHARIBIFU WA MISITU AMBAZO HAZIKO WAZI SANA


ATHARI ZA UHARIBIFU WA MISITU AMBAZO HAZIKO WAZI SANA
Misitu ni uhai kama inavojulikana na watu kwa asilimia kubwa na pia ikiwa ndio kauli mbiu ya wakala wa huduma za misitu Tanzania  TFS. Zamani uhitaji wa kupanda miti haukuwepo kutokana na kuwa misitu ilikuwa mingi na matumizi yalikuwa yako chini kutokana na idadi ya watu lakini pia maendeleo yanayohitaji bidhaa hizi za misitu kama malighafi za kuzalishia bidhaa hizo. Kwa kipindi tulichopo sasa kutokana na hali halisi kubalika tumeingia katika janga la kupoteza misitu kwa asilimia kubwa sana na hali hiyo kupelekea kuwa na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kupelekea kuwa na mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti kwa kiasi kikubwa na kulida misitu ile ambayo bado imesalia kusudi isiweze kuvamiwa tena. Na ahgenda hii imekuwa ya kimataifa kwani na Afrika kuwa mhanga mkubwa wa mabadiliko ya tabia nchi lakini nchi nyingine zote duniani nazo zanpatwa na madhara hayo kwa namna moja au nyingine.  
Athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo husababishwa na uharibifu wa mazingira hasa uharibifu wa misitu ambazo wengi tunazifahamu ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa mvua ambayo husababisha ukame mkubwa na kukausha mimea lakini pia kuharibu makazi ya viumbe hai kama ndege na vinginevyo. Joto kuongezeka na kusababisha mgonjwa ya Ngozi na madhara mengine ambayo hayakuwepo kabla, ongezeko la wadudu katika kilimo inayopelekea wakulima wa hali ya chini licha ya kuathiriwa na ukame ila hata kule kidogo ambacho wanakipata huharibiwa na wadudu na kufanya kuwa na uhitaji wa chakula kwa kiasi kikubwa.
Pamoja na athari zote hizo ila kumekuwa na athari moja ambayo ni kubwa ila watu wanashindwa kuitambua kwa urahisi kuwa nayo pia ni kutokana na uharibifu wa mazingira hasa katika eneo la uoto wa asili “Biodiversity” hili ni eneo muhimu sana katika kukamilisha kitu tunachoita msitu. Labda tukumbushane tofauti ya hizi aina mbili za misitu na kwann zikatengwa kuwa ni vitu viwili tofauti. Misitu ya asili na misitu ya kupandwa, misitu ya asili maana yake ni miti iliyofungana lakini pia chini kuna uoto unaofunika ardhi “trees with vegetation cover” na msitu wa kupandwa ni miti iliyopandwa kwa nafasi na kupaliliwa na hivyo kukosekana ule uoto unaofunika ardhi.
Aina zote mbili za misitu zinafaida ya kuleta mvua, kukabiliana na tatizo la ongezeko la joto, kunyonya hewa chafu inayotoka viwandani na kupendezesha mazingira yetu. Faida ambayo misitu ya asili inaizidi misitu ya kupandwa ni ile ya uwepo wa uoto wa asili unaofunika ardhi. Hii faida yake huonekana pale mvua inaponyesha utaona katika msitu wa kupandwa maji yanayotiririka ni mengi kuliko maji yanayotiririka katika msitu wa asili. Tofauti hii husababishwa na katika msitu wa asili tone linapodondoka linalazimishwa kuzama chini kwani halipati nafasi ya kuungana na matone mengine kutengeneza maji mengi na kuanza kutembea ila katika misitu ya kupandwa tone linapodondoka linaruka na kupata nafasi ya kukutana na tone jingine na hivyo kutengeneza maji na kuanza kutembembea kuelekea mteremko ulipo na mwisho wa siku hutengeneza mfereji na mwisho korongo na kuleta mafuriko huko mabondeni.
Hata hivyo kinachosikitisha sana kwa sasa hata hii misitu ya asili asilimia kubwa imekuwa kama misitu ya kupandwa na kuwa na tabia za misitu ya kupandwa japo inaundwa na misitu ya asili. Hii yote imetokana na shughuli za kibinadamu zinazofanyka katika misitu hiyo ikiwa kubwa Zaidi ni ufugaji na uchungaji wa mifugo unaoharibu kwa kiasi kikubwa uoto huo wa asili unaofunika ardhi. Hivyo unaweza pita kwa mbali ukaona miti imefunga vizuri ukajua hapo kuna msitu mzuri wa asili lakini ukisogea karibu unakutana na ardhi ikiwa uchi na kuondoa maana yote ya msitu wa asili na kuwa kama msitu wa kapandwa tu.
Kwa mujibu wa wazee wa zamani ambao bado wapo wanasema kuwa hawajashtushwa na mvua hizi kubwa zinazoendelea kunyesha kwa sasa ila kinachowashangaza ni mafuliko yanayotokea kwani hawajawahi kuyashuhudia kabla maana mashamba yanajaa maji n ahata kilimo kimekuwa changamoto kubwa kwao. Wanasema hata mwaka 1998 iliponyesha mvua kubwa ya elninyo maji hayakuwa mengi kiasi hiki ila kwa hii ya mwaka huu imekuwa ya kushangaza kidogo kwao. Hapa ndo unagundua sasa kuwa uharibifu wa uoto wa asili umechangia kiasi kikubwa katika kusababisha maji kutiririka kwa kasi kutoka milimani na kusambabisha mafuriko, uharibifu wa miundo mbinu na majanga mengine mengi.
Ufugaji ni mzuri na una tija kwa wananchi wenyewe na pia kwa taifa kwa ujumla kama ukifanywa kwa kuzingatia usalama wa mazingira yetu hususani katika misitu yetu ya asili. Lakini kama tusipolifanyia kazi hili mapema tutegemee kila mvua zitakapokuwa zinanyesha basi kutakuwa na madhara kadha wa kadha kwa wananchi na hata kwa serikali kwa ajili ya kutengeneza miundo mbinu inayoharibiwa na mvua kila wakati.
Rai yangu kwa mamlaka zinazohusika tunajitahidi kuhamasisha watu kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi tusisahau kuilinda misitu ya asili na uoto wake kwa vyote vina umuhimu mkubwa sana kwa maendeleo ya taifa na wananchi wake kwa ujumla. Hivyo kila mtu apande miti mingi kadri anavoweza lakini pia tuwajibike wote katika kuitunza misitu ya asili iliyopo kusudi kuepukana na haya yote yanayotokea sasa hivi.
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika.
Imeandika na Martin Njau,
0717599375/0753989840 njaumartin48@gmail.com
Mwanaharakati wa mazingira na bwana Misitu.

Jumamosi, 11 Agosti 2018

DO LITTLE FOR MORE CHANGES

Katika maisha ya binadamu watu wengi wanaogopa au kuona kuwa unapofanya kitu kidogo hakina maana katika mazingira flani, lakini ipo siri kubwa katika kufanya kitu kidogo kinachoweza kukuletea mafanikio makubwa sana hadi ukashangaa.
Kila siku tunazungumzia juu ya mabadiliko ya tabia nchi na kila siku yanazidi kuleta athali kubwa kwa jamii na taifa kiujumla.
Lakini ipo njia ambayo tunaweza kuanza na mwisho wa siku tukajikuta tunapata matokeo mazuri na makubwa.
Hebu fikiria kama ukijiwekea ratiba ya kupanda miti kumi kila msimu wa mvua ambao kwa kawaida huwa ipo miwili unaweza kuona ni kitu kidogo ila kwa mwaka utakuwa umepanda miti 20 kwa miaka mitano ni sawa na miti 100 kwa watu 100 ni sawa na miti 10000 na kuendelea sasa utaona ni jinsi gani unaweza kufanya jambo dogo ila mafanikio yakawa makubwa.
Let's start now, hatujachelewa climate change elimination is possible.

Jumatano, 6 Desemba 2017

“TELL THEM TO PROTECT ME AND I WILL PROTECT THEM TOO”



TELL THEM TO PROTECT ME AND I WILL PROTECT THEM TOO
“WAAMBIE WANILINDE NAMI NITAWALINDA PIA

Kulinda, kulindwa, kulindiwa, ulindaji, etc yote haya yanatokana na mzizi wa neno “LINDA”. Linda” ila sio jina la mtu” kwa maana rahisi ni kitendo cha kuwekea ulinzi kitu fulani ili kisipatwe na matatizo au kisisumbuliwe na vitu vingine. Unapotaka kulinda kitu ni lazima ukifahamu kitu chenyewe kwa undani ilkiwa ni pamoja na umuhimu wake kwako ikimaanisha faida zake. Lakini kikubwa ni kuwa unapohitaji kulinda kitu flani lazima ujue njia zipi zinazotumika kukilinda kitu hicho kikamilifu. Hii itakusaidia kupata mtiririko mzuri wa kukilinda kitu hicho ili kuweza kukupatia faida zaidi na zaidi.

Mazingira ni kitu cha muhimu sana katika maisha ya binadamu na ikiwa yanawekwa katika hali ambayo sio salama basi husababisha usalama kupotea pia kwa wale wanaoyatumia. Lakini pia katika mazingira ndio tunapopata vitu vingine vingi ikiwepo pia misitu na mengine mengi ambayo tunayapata pale tunapoweka mazingira sawa.

Lakini hapa ninachotaka kukizungumzia zaidi ni utunzaji wa mazingira kwa ujumla lakini nikiegamia sana katika utunzaji wa misitu yetu. Nadhani wote tunafahamu umuhimu wa kutunza misitu na kila siku tunakumbushana kuhusu kitu hicho ambacho ni faida kwa wote. Ipo sauti inayoita kutoka katika mazingira au katika misitu ikisema kuwa “WAAMBIE WAKINILINDA NAMI NITAWALINDA PIA” hii ndo inayonisukuma kuandika hiki kwenu leo wote wana mazingira kwa ujumla wetu.

Nakumbuka nishawahi kuandika kuhusu kila mtu ni mwanamazingira kwa asili ila kuwa bwana/bibi misitu ni chaguo la mtu kusomea kitu hicho. Hii ilikuwa na maana kwamba kila mtu anaishi katika mazingira ila wanaishi misituni ni wachache sana na wengi ni wanyama. Hivyo tunapaswa kuwa na elimu ya utunzaji wa mazingira hata bila ya kuipata kutoka darasani kwani ni faida ya kila mmoja wetu katika maisha yake.

Hivi karibuni tumekuwa tukisikia kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea kutokea kila mara na kuzidi kwa kasi. Haya yote yanasababishwa na uharibifu wa mazingira unaofanyika katika maeneo mbalimbali ya dunia. Tumekuwa tushuhudia ongezeko la joto ambalo inakadiriwa kuwa limeongezeka kwa takribani nyuzi 3 hadi 5 na kusababisa kuyeyuka kwa barafu ambazo zipo kwenye milima mirefu kama vile mlima Evarist uliopo bara la Asia na pia mlima Kilimanjaro ambao upo katika nchi yetu.

Description: C:\Users\AUDAX\Desktop\211_shutterstock_372px.jpg

Ila sio hilo tu bali tumekuwa tukishuhudia barafu ya bahari ya atlantiki inavyozidi kupungua na kusababisha kina cha maji kuendelea kupanda na kufunika baadhi ya visiwa ambavyo vilikuwa vinaonekana hapo mwanzo. Hiyo yote ni sababu ya ongezeko la joto ambalo linasababishwa na uharibifu wa mazingira hasa uharibifu wa misitu.  Na huu husababishwa na shughuli mbalimbali za kijamii zinazofanyika katika maeneo ya makazi na hata shughuli za kibiashara kama vile viwanda na pia usafirishaji.

Lakini hali hii mbaya ya tishio kwa taifa na hata kwa dunia nzima ni lazima kuwepo na juhudi za makusudi za kuweza kuipunguza kama si kuitokomeza kabisa. Inawezekana endapo kila mtu atachukua hatua madhubuti juu ya hili ili kupunguza athari hizi zinazoikabili dunia kwa ujumla. Kinachotakiwa kila mtu amfikirie mwenzake kwamba anaumia kiasi gani juu ya uharibifu huu na aifanye hali ile iwe kama yake kwani nchi nyingi zilizoendelea ndio zinaongoza kwa uchafuzi wa mazingira ila madhara mengi huja kwa wale wasio na hatia.

Hivyo basi sote na tuisikie sauti hii inayoita kutoka katika mazingira yetu na hata  katika misitu yetu kuwa tukiitunza na kuilinda basi nayo itatutunza na kutulinda na kutuweka katika hali nzuri isiyo ya hatari na mashaka kama tulivyo sasa. Kwani mvua zitakuwa za kutosha na kwa wakati, maji hayatakuwa na tabu katika upatikanaji wake, joto litapungua ila pia ile barafu iliyokuwa inayeyuka kutoka katika milima mirefu itaacha kuyeyuka tena.

Tuyapende mazingira, tuipende misitu, tuwe marafiki wao kwani tukiwa maadui wao nao watakuwa maadui wetu. Wito wangu kwa kila mmoja ona uchungu kwa kizazi hiki na kile kijacho wasije kuta simulizi tu kwa yote yaliyotokea. Ni wakati wangu na wako kusitisha athari hizi za mabadiliko ya tabia nchi kuendelea kutuumiza. Anza sasa bado hujachelewa tunza mazingira, tunza misitu, panda miti kwa wingi epuka athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Kila mtu na asikie sauti hii inayotoka katika mazingira na misitu ya kuwa “mkitulinda nasi tutawalinda” tukiisikia na kuifanyia kazi basi tutaona mabadiliko.

Kumbuka ustawi wa mazingira na misitu uko juu yangu na yako tuchukue hatua.

Mungu ibariki Afrika

Mungu ibariki Tanzania.


Njau Martin
+255 717 599 375