Jumanne, 21 Machi 2017

HAPPY WORLD FORESTS DAY.

Leo ni siku ya Misitu duniani, na hakuna mtu ambaye hajui umuhimu wa misitu popote pale alipo ikiwa ni kwa kusoma kwenye vitabu, kuambiwa au pia kujionea mwenyewe. Ujumbe wa mwaka huu ni "MISITU NA NISHATI". Ukweli ni kuwa karibia asilimia 80% ya nishati inatokana na misitu hivyo tunatakiwa kujua namna ya kutumia nishati hiyo kwa matumizi endelevu kwani tutakapoitumia vibaya ipo siku tutaikosa na itakuwa shida sana. Tuungane pamoja kulinda na kutunza misitu yetu kwa maendeleo endelevu, tuache tamaa ambazo zitatuletea majonzi baadae
Twende sambamba katika kampeni ya kutokomeza mabadiliko ya tabia nchi na athari zake tusiwaachie tu wataalam wa fani kwani sote tuna uwezo wa kufanya jambo kila mtu kwa nafasi yake.  Kila mtu ajipongeze kwa kuwa mtuzaji mzuri wa misitu na sio kujisifu kwa kuwa mharibifu mbaya wa misitu.  "TANZANIA BILA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI INAWEZEKANA, TUANZE MIMI NA WEWE HALAFU YULE NA WALE" By Njau M au Mtaalam wa Miti  "Happy world forests day"

Jumapili, 19 Machi 2017

YATUNZE NAYO YATAKUTUNZA

Uzuri wa mazingira yetu huletwa na utunzaji mzuri wa mazingira hayohayo yanayotuzunguka.  Na katika kufanya maendeleo lazima tuwe yakinifu katika kujua faida za maendeleo hayo tutakapochagua maeneo sahihi na pia tunapochagua maeneo ambayo sio sahihi pia kuna athari kubwa tu kwetu na kizazi kijacho. Mfano Unapofyeka msitu kwa ajili ya kilimo ni kweli unahitaji kufanya jambo la kimaendeleo ila njia unayotumia au eneo ulilochagua sio sahihi. Kwani utaandaa shamba lako ila kumbuka unategemea mvua ili upate mazao sasa kutokana na uharibifu ulioufanya mvua inakosekana, je umefanya maendeleo au umejirudisha nyuma tena kibaya bora ingekuwa wewe pekeyako ila umerudisha nyuma hata wale wasio na hatia kwani kila mtu atakosa kupata mazao. Hivyo basi tufanye mambo ya kimaendeleo ikienda sambamba na kuheshimu mazingira yetu ili nayo yatutunze.  "TANZANIA WITHOUT CLIMATE CHANGE EFFECTS IS POSSIBLE, IT BEGINS WITH ME AND YOU" By Mtaalam wa Miti.  Follow me kupitia blog yangu ujifunze zaidi  "njaumartin. blogspot. com"

Ijumaa, 17 Machi 2017

THINK GREEN ALWAYS IT PAYS

Tunateseka na kupata madhara kwa vitu ambavyo hatujafanya sisi. Athari za mabadiliko ya tabia nchi kila mtu anazifahamu ila chanzo chake kikubwa ni ongezeko la hewa ukaa (Green house gasses)  ambazo hutokana na hewa chafu ya viwandani ambayo kiukweli kwa Tanzania au Afrika kwa ujumla kama ni kuchangia basi ni asilimia ndogo sana. Ila kama baba alikuwa masikini kwa kutokufanya kazi au kuwa na matumizi mabaya ya hela mtoto hutakiwi kila siku kulalamika kuhusu baba yako ila inatakiwa ujipange na maisha yako ujue yataendaje kwani teari ya kwake yameenda mpaka akafikia umri huo. Hivyo basi ni jukumu letu sote kuona kuwa tunapambana na hizi athari kwa njia ambazo zinaweza kutukomboa kama vile kupanda miti kwa bidii sana,  kuepuka kukata miti ya asili kwani ina msaada mkubwa katika kupunguza hewa ukaa, kulinda vyanzo vyetu vya maji kwa kutolima katika vyanzo vya maji, kuelimishana juu ya athari hizi kwa vizazi vijavyo na kikubwa kulinda na kutunza misitu iliyopo kwa maendeleo endelevu. Kwa pamoja tunaweza tuamke tuanze kazi. Athari za mabadiliko ya tabia nchi zinaweza kupunguzwa na kuondolewa kabisa.  Tambua "FORESTS CONSERVATION IS THE SOLUTION FOR CLIMATE CHANGE"  By Mtaalam wa Miti.

FAIDIKA BILA KULETA ATHARI

Hii ni faida ambayo hutokana na uvunaji wa miti ambayo hutupatia hela nyingi.  Lakini faida hii huwa kilio endapo tunaipata kutoka katika misitu ya asili ambayo haitakiwi kuvunwa kwani kwa kufanya hivyo tunazidi kuongeza athari za mabadiliko ya tabia nchi.  Hivyo faida hupatikana kwa kupanda miti sisi wenyewe na kwa sasa wataalam wametuwezesha kuweza kupata mazao haya kwa muda mfupi tofauti na mwanzo unapanda anakuja kuvuna mtoto wako kwa sasa unapanda mwenyewe na unavuna ukiwa bado una nguvu.  Tushirikiane kutokomeza uvunaji wa miti katika misitu ya asili hebu tupande miti ili tupate faida na kujikinga na mabadiliko ya tabia nchi. Tuache ukatili kwani mimi na wewe tutapata hela leo lakini itakuwa kilio cha mda mrefu kwa watoto wetu. Tuwapende na kuwathamini kizazi kijacho.  Ungana nami kwa kusambaza ujumbue huu pia like na comment kuongeza ufanisi.  TANZANIA WITHOUT CLIMATE CHANGE EFFECTS IS POSSIBLE, IT BEGINS WITH ME AND YOU" By Mtaalam wa Miti

Jumapili, 5 Machi 2017

USIFANYE JAMBO KWA KUWA KUNA KUFANYA.....



“USIZAE WATOTO KWA KUWA KUNA KUZAA, ILA ZAA KWA KUWA UMEANDAA MAZINGIRA YA KUPOKEA MTOTO”
“DON’T HAVE A CHILD COS WE HAVE BEEN TOLD TO HAVE THEM, BUT HAVE A CHILD YOU ARE ABLE TO CARE HIM/HER”
Ni ukweli usiopingika kuwa upo wakati unafanya vitu ambavyo kwa hali ya kawaida sio kwamba umefikiria kwa makini ni kwanini unafanya hilo jambo ila labda ni kutokana na mazoea au kutokana na tamaduni za jamii fulani au pia kutokana na nani amefanya nini. Hii hutupelekea kufika sehemu na kujikuta tukisababisha maumivu kwa wengine either indirect or direct kwa kuwa wale ambao wanakuwa assosiated na hivi vitu huwa wanapata shida eneo fulani na kujikuta wanaathilika bila kuwa na hatia.  
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba unapofanya kitu chochote hakikisha ya kwamba umeshaweka mazingira thabiti ya kuonesha kweli kile unachofanya umekitafakari na hujakurupuka kukifanya tu. Hii itakusaidia kuepusha baadhi ya mambo ambayo hayana ulazima kujitokeza na kuathili watu na mfumo wa maisha. Mfano suala la kupata watoto ni jambo zuri ila ni lazima ufikirie kwanza ni kwanini unataka kupata mtoto na je umemuandalia mazingira ya kuja kukaa kwa raha?
Yeye anapokuja hajui chochote kuhusu duniani na anatarajia kuja kuiona dunia nzuri na tamu ,ila pale inapotokea tofauti huwa kwake ni shida kwa kuwa hakutegemea hilo. Kama ww ulisoma kwa shida basi haimaanishi na mtoto wako nae asome kwa shida hivyohivyo ila inatakiwa basi umuandaliea mazingira ambayo yanaweza kumfanya awe na furaha na asione kama duniani ni sehemu mbaya kwake basi sehemu nzuri na yenye amani tele.
Nakazia sana katika suala la kupata mtoto kwa kuwa ndio sualal ambalo wengi huwa wanakosea na kujikuta wanajilaumu baadae kuwa ni kwanini walifanya hivyo. Haina haja ya kujilaumu baada ya muda ila kinachotakiwa kuwepo ni kuwa makini kuanzia mwanzo ili kuepuka matatizo ambayo yanaweza kujitokeza kwa namna yoyote ile labda itokee bahati mbaya sana. Usilete dhana ya kwamba kwakuwa mm nimesoma kwa vidumu so hata mwanangu anatakiwa asome kwa vidumu,  hatuishi kwa mazoea basi tunatakiwa tuishi kutokana na mazingira husika yalivyo.
Ila sio jambo hilo yapo mengi ambayo hatuna budi kuyaangalia ili kuweza kuweka mambo sawasawa. Hivyo kikubwa katika maisha ni bora uwe na moja uliyo na uwezo nayo kuliko kuwa na kumi ambazo huna uwezo nazo. Logic behind ni kwamba ridhika na unachokipata kwa muda husika na muombe Mungu akujalie zaidi kwa wakati wake kwani yeye ndo hujua wakati uliosahihi kwetu na wakati usio sahihi kwetu kwa ajili ya kutupa neema zake.
“ALWAYS BE GOOD TO THE PRESENT AND THE FUTURE"
njau martin
njaumartin@gmail.com
0717599375

ISHI KUTOKANA NA JAMII ILA USITENDE DHAMBI



“ISHI KUTOKANA NA MAZINGIRA LAKINI USITENDE DHAMBI”

“LIVE ACCORDING TO THE ENVIRONMENT BUT DO NOT SIN”

Habari siku ya leo mpendwa wangu ,ni matumaini yangu kuwa u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Napenda kumshukuru mungu kwa kutulinda na hatari zote na kutufikisha hapa tulipo, kwani ni wengi walipenda kufika ila hawakuweza ila kwa sisi tuliofanikiwa kufika basi tutambue kuwa si kwa uwezo wetu bali ni kwa uwezo wa yule aliyetuumba.

Karibuni tena katika safu yetu ya kushirikishana vitu mbalimbali vinavyohusu mambo mbalimbali ya kijamii na jinsi ya kuishi kwa furaha na amani na jamii inayotuzunguka. Leo napenda tushirikishane kitu kimoja ambacho ni “kuishi kutokana na mazingira au jamii lakini usitende dhambi”

Watu wengi husema kuwa maisha ni kwa ajili yangu na hivyo kila ninachokifanya kinakuwa na implication kwangu tu na sio kwa mtu mwingine. Hiyo sio sawa na naomba tuifute hiyo dhana katika vichwa vyetu kwani inapoteza kabisa. Ukweli maisha sio yako peke yako bali maisha unatakiwa uishi kwa ajili ya wengine. Kwa wale wakristu tunaamini kuwa mwanadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa adam na huyo Mungu alimuumba kutoka kwenye udongo. Ila Mungu mwenyewe akaona sio vyema kwa adamu kuwa peke yake akamfanyia msaidizi wa kufanana nae, hebu fikiria kama ungekuwa pekeyako katika dunia hii ingekuwaje, nikiwa na maana ya kwamba hakuna wazazi wala walezi wala mtu yeyote yule , nadhani maisha yangekuwa magumu sana kwani upweke ungetawala sana hivyo kumbe Mungu hakukosea kumfanyia adamu msaidizi wa kufanana nae.

Inashangaza sana mtu anakuambia kuwa Mungu anaangalia moyo tu ,kama ni hivyo mbona Mungu aliwafanyia nguo za magome ya miti adamu na hawa walipoasi unahisi alikuwa anaonesha nn? Labda unahisi alikosa kazi ila sivyo alikuwa na maana kuwa japokuwa yeye anaangalia moyo lakini moyo upo ndani ya nn?
 Na je kuna uhusiano gani kati ya moyo na mwili? Tuangalie mke wa ruthu aligeuka jiwe la chumvi , swali ni kwann haukugeuka moyo tu jiwe la chunvi ukageuka mwili mzima? Pia katika hali ya kawaida tunaona kuwa pale moyo unapoumia viungo vyote vya mwili huweza kupata ile athari iliyokuwapo kwenye moyo je ushawahi kujiuliza ni kwanini inakuwa hivyo?
 Ukweli ni kwamba ukatae usikubali upo uhusiano mkubwa sana kati ya moyo na mwili. Na katu moyo hauwezi kuwepo bila mwili vivyo hivyo mwili bila moyo.

Ukiangalia kwa makini utaona kuwa tunatakiwa tuishi pasipo kuwa vikwazo kwa watu wengine. Unaweza kuwa kikwazo kwa watu wengine either kwa kujua au kwa kutokujua ndo maana nikaita somo hili ni kuishi kutokana na jamii husika au mazingira husika lakini usitende dhambi. 
 Papa fransis amewahi kusema “life lived without others is not a life” Unapomkwaza mwenzako na kumpelekea either kutenda dhambi au kumsogeza karibu na mazingira ya kutenda dhambi basi nadhani adhabu yako unaijua ya kwamba ni bora ufungiwe jiwe la kusagia shingoni na ukatupwe baharini sio maneno yangu bali ni maandiko matakatifu ndio yanatuelekeza hivyo. Sasa ndugu yangu acha dhana ya kwamba hata nikivaa vibaya , nikitukana sana ,nikilewa sana ili mradi simfanyii mtu direct ikiwa na maana kumtukana mtu au kunywa pombe kwa ajili ya mtu au kuvaa vibaya kwakuwa tu umependa eti kwa kuwa Mungu haangalii ya nje umepotea kumbuka unachofanya ndio kinachokuonesha jinsi ulivyo ndani mwako hivyo tuwe makini na vitu ambavyo tunavifanya kwa kuwa hututambulisha kwa watu wengine bila sisi wenyewe kujua.

Inatupasa tutambue kuwa ile amri ya kwamba mpende jirani yako kama nafsi yako ina upana sana na haiishii tu katika kusaidiana ki material things ila hata kiroho ndio zaidi. Hapa namaanisha unapofanya mwenzio akafa kiroho ujue una kitu cha kujibu kwani hapo hakuna upendo tena bali ni chuki na kutaka mwenzako nae aende motoni kama ww ulivyochagua. Samahani usije ukanikariri vibaya kwamba ninakuhukumu la hasha unajihukumu mwenyewe kwa matendo yako. Mimi wajibu wangu ni kukumbusha tu nn unatakiwa kufanya.

Tunapoambiwa tuwapende jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe ina maanisha kuwa tuwasaidie pia kutoingia majaribuni na kuwaokoa pale wanapoingia kwa bahati mbaya ila sio kufurahia kuwa ngoja tumuone alikuwa anaringa sana sasa amepatikana hapana hatupaswi kuishi hivyo. Na ndio maana tuna jukumu la kuishi kwa ajili ya wenzetu na sio sisi peke etu kwani kwa maisha hayo hayatatusaidia kufika kule ambako Mungu ametuandalia tufike.

Hakika tukiishi kwa ushirikiano tutaweza kutimiza yale ambayo Mungu ametuelekeza tufanye na hakika tutaishi kwa amani sana huku kila mmoja akiwa na ari ya kumtumikia Mungu kwa nguvu zote na kuikimbilia ile ahadi tuliyoahiwa naye Mungu wetu. Mwenyezi Mungu atubariki sote na kutuangazia uso wake na baraka zake zikawe nasi daima.

“BE BRAVE MORE THAN SNAKE BUT HAMBLE AS DOVE”

Njau martin

Mtaalam wa miti.

0717599375

Njaumartin48@gmail.com