Jumanne, 31 Januari 2017

LOVE WHAT YOU GET



SOMETIME YOU HAVE TO LOVE WHEN YOU GET IT OR YOUR SURE OF GETTING IT”
“WAKATI MWINGINE INABIDI UPENDE BAADA YA KUPATA AU KUWA NA UHAKIKA WA KUPATA “
Ni matumaini yangu kuwa u mzima wa afya na unaendelea vizuri na shughuli za ujenzi wa taifa hili. Na kama utakuwa pia hufanyi hivyo basi utafanya kazi ya kusifia kuwa taifa limependeza au dunia imependeza japokuwa hujashiriki kuipendezesha ila kutokana tu labda na maombi yako basi tumefika hapo tutakapokuwa. Katika maisha hakuna mtu ambaye hana upndo wa dhati japokuwa hutokea wakati ukaingia doa kutokana na mabonde na milima ya hapa na pale ambayo katika maisha ni kitu cha kawaida. Wapo ambao walishasema na hata kujifanya wanaapa kuwa hawatapenda tena ila mwisho wa siku ndio wanakuwa wapendaji wazuriri sana watoto wa mjini tunasema unaingia baharini kwa miguu yote miwili hauna wasiwasi wa mamba wala kiboko kwakuwa unajihisi ni mamba ya ya mamba na kiboko zaidi ya kiboko. Kiukweli ni nzuri na inafurahisha lakini lazima uangalie nguvu ya kubadilisha moja kuwa saba na saba kuwa moja je ni sawa au ipi rahisi.
Hakuna kitu kizuri kama kupenda asikwambie mtu kwa kuwa unaweza hisi una uweza wa kupigana na simba dume  mwenye njaa bila silaha yoyote na ukamuua bila hat akupata jeraha lolote mwilini. Kwa uhalisia ni kama ndoto ila kiimani inawezekana kabisa tena ni kitu kdogo sana. Kama wote tungeweza kuwa na imani kama hizi za kupigana na simba na kumuua bila kupata jeraha lolote hakika ingekuwa vizuri sana ila kutokana na uhalisia na story tunazosikia juu ya ukali wa simba huwa tunajikoki sana na mwisho wa siku inakuwa tunavizia akitotea tu ndio tunafanya mambo na wakati mwigine woga wetu hutufanya kurudi na majeraha ambayo wakati mwingine hata hayatokani na simba labda kutokana na woga wetu ambao tumekuwa nao na kujikuta tukikwarza kwenye miti na hata kuanguka.
Ila ninachoamini mimi ni kwamba porini hayupo simba peke yake wapo wanyama wengi wapole na wanyenyekevu kama tembo twiga swala na wengine wengi ila tatizo letu tunapoenda tunahisi kukutana na simba tu na pia hatufikirii kuwa simba haishi kila sehemu ana maeneo yake maalum ya kuishi. Hivyo makosa yetu ni kufikiria kuwa porini wapo simbatu na hata pale anapotokea swala au hata sungura unatumia nguvu zilezile za kupambana na simba kupambana nae na hapo ndipo hupandikiza roho ya usimba juu ya viumbe hawa wadogo na baada ya hapo wanakuwa kama simba lakini kiuhalisia sio.
Hapa nataka kumaanisha kuwa hakuna mwanamke yeyote au mwanaume yeyote anayependa kuumizwa au kumuumiza mwenzake na kama ingekuwa hivyo mbona zamani watu walikuwa wanaanza urafiki ,uchumba ndoa mpaka wanazeeka pamoja bila shida yoyote. Ila kwa sasa utasikia ooh kaondoka kaenda kwao, mara hajalala ndani wiki moja ,mara hahudumii watoto n.k. Na bora hata mkifika huko mmejitahidi wengine maskini wanaishia kuitwa wapenzi tu hata hatua ya kuitwa mchumba bado na anatarajia kuzeeka ,na wengine wanaishia kuitwa wachumba tu unajiuliza hivi miaka hii ndoa hufungwa baada ya miaka kumi maana kila siku unatambulishwa tu ya kama kozi ya darasani kila mtu akipitia pale anafundishwa then akihama darasa haondoki nayo anaiacha hapohapo. Inasikitisha na inakatisha tamaa.
Lakini hebu tuangalie tatizo liko wapi na nin chanzo cha tatizo hilo? Kuna vitu viwili hapa ambavyo ningependa kuwashirikisha. Kimoja ni kwamba huwa tunapenda sana kwanza kabla hatujajua kuwa je tutafanikiwa au la.Sisemi kuanza kupenda kitu kabla hujakipata ni kosa naomba nieleweke hivi kuwa kupenda kitu sana kabla hujakipata au huna uhakika wa kukipata ni sumu. Utaniuliza sumu kivip? Sumu kwasababu wew utakuwa mipango yote na jitihada zako zote zitakuwa juu ya kitu hicho na mwisho wa siku unapokikosa nadhani unajua nn hutokea, wanaita mvulugano wa kifikra hivyo unachoona chochote mbele yako ili kuondoa machungu ya kukikosa kile cha mwanzo basi wew nacho then kama hukuwepo eneo la tukio. Ni imani yangu kuwa tupo pamoja katika mada hii najaribu kutumia lugha nyingine ila mantikia ya somo hili ni kuhusu swala zima la mapenzi kati ya mwanamke na mwanaume.
Kitu kingine ni kwamba kutokana na ile dhana tulionayo  kuwa porini wanakaa simba tu basi tunapoenda tunahisi kukutana na simba tu. Namaanisha tuna dhana ambayo haitufanyi tukaaminiana mwanamme anasena mwanamke hatuliagi hata siku moja na huku nako mwanamke anasema wanaume wote baba yao mmoja akimaanisha tabia zao zinafanan ambazo ni mbaya zote. Nahisi unaweza ukapata picha juu ya mechi hii ya mahasimu wawili inaishia kwa matokeo gani kwani kila mtu amejiandaa vya kutosha kupiga mshambulizi ya kufa mtu.
Sasa kibaya zaidi ni pale wanapokutana mwanamke ambaye hana hizo athari za mawazo hayo ila mwanamme aliye nae anazo hivyo baada ya mwanaume kula kona ndo mwanamke nae anashituka kwamba kumbe ndo kulivyo hivyo na yy anajipanga sasa unaweza ukaona hii chain itaishia wap. Sasa kipi cha kufanya?
Acha kumpenda sana kabla hujampata au huna uhakika wa kumpta kwani utakapomkosa utaumia sana na ndio chanzo cha mengine yote kutokea. Narudia tena simaanishi usimpende kwani mwanaume hawezi mfuata mwanamke kabla hajavutiwa nae na kumpenda na vivyohivyo mwanamke kwa mwanaume. Ila ninachoshauri mimi “USIMPENDE SANA UKAMFANYA KILA KITU KWAKO” wakati hujampata na wala huna uhakika wa kumpata otherwise utalazimisha uvunje uhusiano wao au wewe mwenyewe ufanye mambo ambayo hayapo.
Pia tuache mawazo ya kwamba kila mwanamke au mwanaume ni mhuni au sio mwaminifu kwenye mapenzi kwani tukifanya hivyo nani atabaki sasa cos wote tutakuwa at the samw pot hivyo hatutafika popote kwa hali hiyo. Tambua mapenzi ni matamu unapopendwa ila ni noma pale unapotendwa au usipopendwa wakati teari wewe ulishaweka malengo mengi juu ya mtu huyo.
“REMEMBER LOVE CAN MAKE U LIVE AND THE SAME LOVE CAN LET U GO BE CAREFUL “
NJAU MARTIN R
MTAALAM WA MITI
njaumartin@gmail.com
0717599375

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni