Jumanne, 31 Januari 2017

PENZI LA MWANZO



PENZI LA MWANZO NI KAMA ARDHI AMBAYO HAIJAWAHI KUTUMIKA
Mwaka ndo unakamilika na tunatarajia kuanza mwaka mpya ambao waswahili wanasema mwaka mpya na mambo mapya. Msemo huu haumaanishi kuwa tuache kila kitu tulichokuwa tunafanya mwaka huu na tuanze vitu vipya hapana ila ni kuwa na mipango ile yenye mafanikio na kuongeza mingine ya kujiendeleza.
Thamini sana penzi lako la mwanzo kwani huwa ni la dhati na la kweli. Penzi hili hufanana na ardhi ambayo haijawahi kulimwa hata mara moja na pale inapoanza kulimwa mazao yake huwa ya kipekee sana tofauti na miaka yote itakayofuata. Moyo ni kiungo ambacho huwa hakipendi usumbufu sana ni sawa na mtoto mdogo unapomfundisha kitu hukishika sana tofauti na akiwa mkubwa. Moyo hupokea kwa dhati upendo ule ambao huja kwa mara ya kwanza na kujiaminisha kuwa ndio pekee na hakuna mwingine kama huo. Ila inapotokea upendo ule ukafa au kuondoka moyo huwa na wasiwasi na hapo ndipo akili huchukua jukumu la kufundisha moyo kupokea upendo tena na ikibidi kuulazimisha kupenda kitu ambacho ni hatari sana katika tasnia nzima ya mapenzi. Thamini penzi lako la mwanzo pia mthamini yule ambaye moyo umekubali kumpokea kwa mara ya kwanza wakati ukiwa pure. Kama tutajitahidi kuwa hivi basi maumivu katika mapenzi hayatakuwepo na itakuwa amani tu.
NOTE                                                                  
Kumbuka moyo haufundishwi kupenda wala kulazimishwa kupenda inapofikia hatua hiyo jua kuna tatizo sehemu na kuwa makini sana katika hilo kwani majuto anaweza kuwa jirani yako au ndugu yako kabisa.
EPUKA KUWA SABABU YA FULANI KUCHUKIA MAPENZI NA HATA NDOA KWANI NDOA NI AGIZO KUTOKA KWA MUNGU NAYO IHESHIMIWE NA KILA MTU
“WISH YOU HAPPY NEW YEAR 2017”
NJAU M
FOREST VOICE {PF}
0717  599375

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni