Jumanne, 31 Januari 2017

ONLY ME NO ONE ELSE



THE MOMENT YOU FEEL LIKE THE WORLD IS FOR YOU ONLY AND NO ONE ELSE
Maisha ni kitu cha ajabu sana kiasi kwamba kila mtu huwa na namna yake ya kuyaelezea maisha kutokana na uelewa wake, mambo mbalimbali aliyopitia na baahdi ya watu aliowahi kuishi nao kwa wakati Fulani. Ila hufika wakati maana hiyo ya maisha ambayo alkikuwa nayo au alikuwa anaifahamu na kuamini kuwa ngio maana kamilili na hata kuona kuwa za wengine ni uongo au mbwembwe tu hubadilika na kuwa tofauti kabisa na mwanzo. Ila hufika wakati mtu huyo kuanza kujiuliza kuwa ilikuwaje mwanzo nikawa na maana ile na sasa hivi nina maana nyingine jibu huja ni kutokana na mazingira husika yanayomzunguka mtu huyo.
Ila ninachoamini mm ni kwamba maana nzuri na yenye ukweli katika maisha huja pale unapolkuwa katika wakati flani ambao hukuwaza kabla kama utakuja kuwa katika wakati kama huo. Nadhani utakuwa unajiuliza maswali mengi kwamba nn maana ya maneno haya ninayosema na kipi kinanifanya nipate uwezo wa kuongea maneno haya. Kamwe huwezi simulia vizuri maumivu ya kun’gatwa na nyoka kama hujawahi kun’gatwa na nyoka hata siku moja. Na ili ujue vizuri vizuri utamu wa mapenzi lazima uwe umeumizwa sehemu out of that it is difficult to realize the potentiality of a thing while you still with it. Simaanishi kuwa lazima kipotee kwanza ndo ujue bali lazima upate shida ya kile kitu ndo utajua vizuri. Mfano huwezi tambua umuhimu wa jembe kama haulimi au unalima ila sio kwa kwa kutumia jembe la mkono.
Kila binadamu hupitia mambo mbalimbali ambayo kwa upande mmoja humpa njia ya kujifunza mambo Fulani katika maisha ila kwa upande mwingine humfanya apoteze hata ule uwezo alionao katika ufanisi wa mambo kwani hujikuta kana kwamba anaelemewa sana na mambo yanayomzunguka na kuhisi kuwa dunia ni ya kwake peke yake. Mimi binafsi nakiri hilo kwani kwa kwa mambo ambayo yamenitokea katika mwaka huu wa 2016 kiasi flani sio rahisi kusema kwamba ni mambo ya kawaida bali mwisho wa siku tunasema inabidi umshukuru Mungu kwa kila jmbo kwani yy ndie mtoaji wa yote hapa duniani. Lakini bado unaweza kujiuliza kitu kuwa tunaamini na tunajua kuwa Mungu wetu ni muweza na ana upendo kwa wote ni kwann huwa anaruhusu masononeko kwa wana wake na kwann anruhusu mabaya yawapate wale anaowapenda?
Unaweza kuona watumishi wa Mungu wengi wanaofanya kazi yake kwa bidii na kikamilifu nao hufika wakati nao wanapatwa na magumu katika maisha je ni kwanini? Nabii isaya anatuambia kuwa ni vigumu sana kuzitambua njia za bwana kwani zipo juu sana na mawazo yake yapo juu sana hivyo sio rahisi kutambua maana ya mambo yanayotokea katika ulimwengu huu pasipo kumshirikisha roho mtakatifu. Mungu huwa na njia nyingi sana katika kuwaelekeza watu wake juu ya mambo ambayo wanapaswa kuyafanya duniani. Pale unaposogea hatua moja na mtu akakurudisha hatua mbili nyuma huwa ni changamoto sana hasa kwa maisha ya sasa hivi. Ukweli mwaka huu wa 2016 umekuwa mwaka wa changamoto sana kwangu kwani ukiachilia mbali kitendo cha kuibiwa pc siku ya jumapili nikiwa nipo kanisani unaweza kujiuliza inakuwaje unaenda kuabudu halafu Mungu anaruhusu mambo kama hayo kutokea. Lakini ikiwa hiyo haitoshi bado nimekuwa nikipata shida za hapa na pale kdili siku zinapoenda kuna wakati nimepata shida ya kutokuelewa ninachosoma hadi nikamfuata sister rosermistica kwa ajili ya ushauri.
Mnamo tarehe 02 december siku ya ijumaa nikiwa natoka misa ya asubuhi kanisani nilikuta ujumbe kwenye simu yangu ya kuwa bibi yangu wa moshi Mungu amemuita kutoka dunia hii. Nilihuzunika kama binadamu mwenye hisia na moyo wa nyama unavyoweza kupokea mambo. Nikiwa kwenye mipango ya kujiandaa kwa ajili ya kuondoka kusudi niweze kwenda kushiriki katika mazishi ya bibi hapo jumanne kama ilivyokuwa imepangwa nikapata tena taarifa ya kutokea kwa msiba wa babu upande wa mama. Nilipata kigugumizi ila nikayapokea yote kama mwanaume ambaye natakiwa kujikaza ili niweze kufanya mambo mengine. Nikafanikiwa kujiandaa na kusafiri siku ya jumatatu na kufika moshi kwa ajili ya kuhudhulia mazishi ya bibi. Lakini asubuh ya siku ya jumanne ambayo ndio siku ya mazishi yenyewe ndio nikapata tatizo jingine la kuibiwa simu yangu aina ya tecno c8. Ukweli kwa wakati ule niliona kama jambo la kawaida kwani bado nilikuwa na maumivu ya misiba yote miwili hivyo sikuona kama ni kitu cha kuniumiza sana kwa wakati huo.
Tulifanya juhudi za kuweza kuitafuta ili angalau kama inaweza kuonekana ila mpaka ninaondoka kule siku ya jumatano asubuh ilikuwa bado haijapatikana na juhudi ya kuitafuta ili kujua inaweza kuwa wapi bado zinaendelea na naamini Mungu zitazaa matunda kwa wakati unaompendza Mungu mwenyewe. Nilifanikiwa kufika kwamgwe salama na kuwakuta baadhi ya watu wameshaondoka ila waliokuwepo tulisalimiana na nikaenda kuona mahali babu alipopumzishwa pamoja na kusali . nikarudi na kuendelea na mambo mengine kabla ya kuondoka kesho yake kwa ajili ya kurudi chuoni kuendelea na majukumu ya kielimu kama tulivyochagua kuwa.
Lakini ukweli nimekuja kupata maumivu ya simu ile niliyoipoteza baada ya kutoka moshi na imenisumbua sana na kujikuta nikikumbuka mambo mengine mengi yaliyopita ikiwa ni pamoja na mtu ninatemdai kiasi cha pesa milioni moja na laki sita ambazo mpaka sasa sijajua kama atanilipa au la, na hayo yote yamekuwa ya  kiniongezea mawazo siku hadi siku. Sasa hapo ndo unaweza kuona kuwa mtu huyu unapomuuliza nn maana ya maisha atakupa jibu gani. Inafikiwa wakati hadi unapomuona mtu anacheka unajiuliza hivi huyu anacheka nn au kwann anacheka wakti mm mwenyewe nakitafuta kicheko hicho ila sijakipata bado. Unatamani kupata mtu wa kukufariji lakini unajikuta kuwa yupo mbali sana au hayupo kabisa so unakuwa katika wakati mgumu sana kimawazo na kifikra pia.
Ila kikubwa ni kumtegemea Mungu tu kwani ndiye mweza yote hapa duniani na kila wakati hutuombea mema na inawezekana hutupa haya ili atuepushe na mengine ambayo yangeweza kuwa mabaya sana kwetu na hata kwa wenzetu wanaotuzunguka. All in all we say thanks for everything because the one who give he knows us more than what we know him. Therefore as we faithful children of God we should be humble in praying so as our God may give us strength and courage of moving on without any worry on the way.
Njau martin R
Forest Voice {FV}
0717599375
GRORY BE TO GOD FOREVER AND EVER
AMEN

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni