“ISHI
KUTOKANA NA MAZINGIRA LAKINI USITENDE DHAMBI”
“LIVE
ACCORDING TO THE ENVIRONMENT BUT DO NOT SIN”
Habari siku ya leo
mpendwa wangu ,ni matumaini yangu kuwa u mzima na unaendelea vyema na majukumu
yako ya kila siku. Napenda kumshukuru mungu kwa kutulinda na hatari zote na kutufikisha
hapa tulipo, kwani ni wengi walipenda kufika ila hawakuweza ila kwa sisi
tuliofanikiwa kufika basi tutambue kuwa si kwa uwezo wetu bali ni kwa uwezo wa
yule aliyetuumba.
Karibuni tena
katika safu yetu ya kushirikishana vitu mbalimbali vinavyohusu mambo mbalimbali
ya kijamii na jinsi ya kuishi kwa furaha na amani na jamii inayotuzunguka. Leo
napenda tushirikishane kitu kimoja ambacho ni “kuishi kutokana na mazingira au jamii lakini usitende dhambi”
Watu wengi husema
kuwa maisha ni kwa ajili yangu na hivyo kila ninachokifanya kinakuwa na
implication kwangu tu na sio kwa mtu mwingine. Hiyo sio sawa na naomba tuifute
hiyo dhana katika vichwa vyetu kwani inapoteza kabisa. Ukweli maisha sio yako
peke yako bali maisha unatakiwa uishi kwa ajili ya wengine. Kwa wale wakristu
tunaamini kuwa mwanadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa adam na huyo Mungu alimuumba
kutoka kwenye udongo. Ila Mungu mwenyewe akaona sio vyema kwa adamu kuwa peke
yake akamfanyia msaidizi wa kufanana nae, hebu fikiria kama ungekuwa pekeyako
katika dunia hii ingekuwaje, nikiwa na maana ya kwamba hakuna wazazi wala
walezi wala mtu yeyote yule , nadhani maisha yangekuwa magumu sana kwani upweke
ungetawala sana hivyo kumbe Mungu hakukosea kumfanyia adamu msaidizi wa kufanana
nae.
Inashangaza sana
mtu anakuambia kuwa Mungu anaangalia moyo tu ,kama ni hivyo mbona Mungu
aliwafanyia nguo za magome ya miti adamu na hawa walipoasi unahisi alikuwa
anaonesha nn? Labda unahisi alikosa kazi ila sivyo alikuwa na maana kuwa
japokuwa yeye anaangalia moyo lakini moyo upo ndani ya nn?
Na je kuna uhusiano
gani kati ya moyo na mwili? Tuangalie mke wa ruthu aligeuka jiwe la chumvi ,
swali ni kwann haukugeuka moyo tu jiwe la chunvi ukageuka mwili mzima? Pia
katika hali ya kawaida tunaona kuwa pale moyo unapoumia viungo vyote vya mwili
huweza kupata ile athari iliyokuwapo kwenye moyo je ushawahi kujiuliza ni
kwanini inakuwa hivyo?
Ukweli ni kwamba ukatae usikubali upo uhusiano mkubwa
sana kati ya moyo na mwili. Na katu moyo hauwezi kuwepo bila mwili vivyo hivyo mwili bila moyo.
Ukiangalia kwa
makini utaona kuwa tunatakiwa tuishi pasipo kuwa vikwazo kwa watu wengine.
Unaweza kuwa kikwazo kwa watu wengine either kwa kujua au kwa kutokujua ndo
maana nikaita somo hili ni kuishi kutokana na jamii husika au mazingira husika
lakini usitende dhambi.
Papa fransis
amewahi kusema “life lived without others is not a life” Unapomkwaza mwenzako
na kumpelekea either kutenda dhambi au kumsogeza karibu na mazingira ya kutenda
dhambi basi nadhani adhabu yako unaijua ya kwamba ni bora ufungiwe jiwe la
kusagia shingoni na ukatupwe baharini sio maneno yangu bali ni maandiko
matakatifu ndio yanatuelekeza hivyo. Sasa ndugu yangu acha dhana ya kwamba hata
nikivaa vibaya , nikitukana sana ,nikilewa sana ili mradi simfanyii mtu direct
ikiwa na maana kumtukana mtu au kunywa pombe kwa ajili ya mtu au kuvaa vibaya
kwakuwa tu umependa eti kwa kuwa Mungu haangalii ya nje umepotea kumbuka
unachofanya ndio kinachokuonesha jinsi ulivyo ndani mwako hivyo tuwe makini na
vitu ambavyo tunavifanya kwa kuwa hututambulisha kwa watu wengine bila sisi
wenyewe kujua.
Inatupasa tutambue
kuwa ile amri ya kwamba mpende jirani yako kama nafsi yako ina upana sana na
haiishii tu katika kusaidiana ki material things ila hata kiroho ndio zaidi.
Hapa namaanisha unapofanya mwenzio akafa kiroho ujue una kitu cha kujibu kwani
hapo hakuna upendo tena bali ni chuki na kutaka mwenzako nae aende motoni kama
ww ulivyochagua. Samahani usije ukanikariri vibaya kwamba ninakuhukumu la hasha
unajihukumu mwenyewe kwa matendo yako. Mimi wajibu wangu ni kukumbusha tu nn
unatakiwa kufanya.
Tunapoambiwa
tuwapende jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe ina maanisha kuwa tuwasaidie
pia kutoingia majaribuni na kuwaokoa pale wanapoingia kwa bahati mbaya ila sio
kufurahia kuwa ngoja tumuone alikuwa anaringa sana sasa amepatikana hapana
hatupaswi kuishi hivyo. Na ndio maana tuna jukumu la kuishi kwa ajili ya
wenzetu na sio sisi peke etu kwani kwa maisha hayo hayatatusaidia kufika kule
ambako Mungu ametuandalia tufike.
Hakika tukiishi kwa
ushirikiano tutaweza kutimiza yale ambayo Mungu ametuelekeza tufanye na hakika
tutaishi kwa amani sana huku kila mmoja akiwa na ari ya kumtumikia Mungu kwa
nguvu zote na kuikimbilia ile ahadi tuliyoahiwa naye Mungu wetu. Mwenyezi Mungu
atubariki sote na kutuangazia uso wake na baraka zake zikawe nasi daima.
“BE BRAVE MORE THAN SNAKE BUT
HAMBLE AS DOVE”
Njau martin
Mtaalam wa miti.
0717599375
Njaumartin48@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni