Tunateseka na kupata madhara kwa vitu ambavyo hatujafanya sisi. Athari za mabadiliko ya tabia nchi kila mtu anazifahamu ila chanzo chake kikubwa ni ongezeko la hewa ukaa (Green house gasses) ambazo hutokana na hewa chafu ya viwandani ambayo kiukweli kwa Tanzania au Afrika kwa ujumla kama ni kuchangia basi ni asilimia ndogo sana. Ila kama baba alikuwa masikini kwa kutokufanya kazi au kuwa na matumizi mabaya ya hela mtoto hutakiwi kila siku kulalamika kuhusu baba yako ila inatakiwa ujipange na maisha yako ujue yataendaje kwani teari ya kwake yameenda mpaka akafikia umri huo. Hivyo basi ni jukumu letu sote kuona kuwa tunapambana na hizi athari kwa njia ambazo zinaweza kutukomboa kama vile kupanda miti kwa bidii sana, kuepuka kukata miti ya asili kwani ina msaada mkubwa katika kupunguza hewa ukaa, kulinda vyanzo vyetu vya maji kwa kutolima katika vyanzo vya maji, kuelimishana juu ya athari hizi kwa vizazi vijavyo na kikubwa kulinda na kutunza misitu iliyopo kwa maendeleo endelevu. Kwa pamoja tunaweza tuamke tuanze kazi. Athari za mabadiliko ya tabia nchi zinaweza kupunguzwa na kuondolewa kabisa. Tambua "FORESTS CONSERVATION IS THE SOLUTION FOR CLIMATE CHANGE" By Mtaalam wa Miti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni