Uzuri wa mazingira yetu huletwa na utunzaji mzuri wa mazingira hayohayo yanayotuzunguka. Na katika kufanya maendeleo lazima tuwe yakinifu katika kujua faida za maendeleo hayo tutakapochagua maeneo sahihi na pia tunapochagua maeneo ambayo sio sahihi pia kuna athari kubwa tu kwetu na kizazi kijacho. Mfano Unapofyeka msitu kwa ajili ya kilimo ni kweli unahitaji kufanya jambo la kimaendeleo ila njia unayotumia au eneo ulilochagua sio sahihi. Kwani utaandaa shamba lako ila kumbuka unategemea mvua ili upate mazao sasa kutokana na uharibifu ulioufanya mvua inakosekana, je umefanya maendeleo au umejirudisha nyuma tena kibaya bora ingekuwa wewe pekeyako ila umerudisha nyuma hata wale wasio na hatia kwani kila mtu atakosa kupata mazao. Hivyo basi tufanye mambo ya kimaendeleo ikienda sambamba na kuheshimu mazingira yetu ili nayo yatutunze. "TANZANIA WITHOUT CLIMATE CHANGE EFFECTS IS POSSIBLE, IT BEGINS WITH ME AND YOU" By Mtaalam wa Miti. Follow me kupitia blog yangu ujifunze zaidi "njaumartin. blogspot. com"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni