Leo ni siku ya Misitu duniani, na hakuna mtu ambaye hajui umuhimu wa misitu popote pale alipo ikiwa ni kwa kusoma kwenye vitabu, kuambiwa au pia kujionea mwenyewe. Ujumbe wa mwaka huu ni "MISITU NA NISHATI". Ukweli ni kuwa karibia asilimia 80% ya nishati inatokana na misitu hivyo tunatakiwa kujua namna ya kutumia nishati hiyo kwa matumizi endelevu kwani tutakapoitumia vibaya ipo siku tutaikosa na itakuwa shida sana. Tuungane pamoja kulinda na kutunza misitu yetu kwa maendeleo endelevu, tuache tamaa ambazo zitatuletea majonzi baadae
Twende sambamba katika kampeni ya kutokomeza mabadiliko ya tabia nchi na athari zake tusiwaachie tu wataalam wa fani kwani sote tuna uwezo wa kufanya jambo kila mtu kwa nafasi yake. Kila mtu ajipongeze kwa kuwa mtuzaji mzuri wa misitu na sio kujisifu kwa kuwa mharibifu mbaya wa misitu. "TANZANIA BILA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI INAWEZEKANA, TUANZE MIMI NA WEWE HALAFU YULE NA WALE" By Njau M au Mtaalam wa Miti "Happy world forests day"
Jumanne, 21 Machi 2017
HAPPY WORLD FORESTS DAY.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni